Friday, February 27, 2015

MWIJAGE AFANYA ZIARA KUKAGUA MAFUTA.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (Wa pili kutoka Kushoto) akifuatana na baadhi ya Viongozi wa Kampuni ya Mafuta ya GAPCO kukagua miundombinu ya kuhifadhia mafuta iliyoko eneo la Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri alitembelea Kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na biashara ya mafuta nchini kufanya mazungumzo na kukagua miundombinu inayotumiwa na Kampuni husika.
Meneja wa Kampuni ya Mafuta ya HASS nchini Tanzania, Ali Hassan Ahmed (Kushoto), akisikiliza maelekezo kutoka kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Nishati), Charles Mwijage (aliyeinua mkono) kuhusu utekelezaji wa mambo mbalimbali unaotakiwa kufanywa na Kampuni hiyo, hususan kujenga mahusiano mema na jamii. Wa kwanza Kulia ni Mbunge wa Temeke (Viti Maalum – CCM), Mariam Kisaka.
Joshua Mtunda (mwenye Fulana ya Njano), akizungumza na Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Anaehusika na Nishati), Charles Mwijage (wa Tatu kutoka Kushoto), kwa niaba ya Vijana wenzake wanaofanya biashara ya kusafirisha abiria kwa Pikipiki (Bodaboda) kuhusu msaada wanaohitaji ili kuboresha biashara yao. Vijana hao wanafanya biashara yao eneo la Kigamboni karibu na ilipo Kampuni ya Mafuta ya HASS.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini (Anaehusika na Nishati), Charles Mwijage (wa kwanza – Kushoto), akikagua miundombinu ya kuhifadhia mafuta ya Kampuni ya Mafuta ya PUMA katika eneo la Kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam. Pamoja naye pichani ni baadhi ya Viongozi wa Kampuni hiyo na Maafisa wa Serikali wanaoshughulikia Sekta ya Mafuta.

No comments: