Sunday, March 22, 2015

KENYA KUJENGA UKUTA KWNYE MPAKA WAKE NA SOMALIA.

WAZIRI wa maswala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery amesema kuwa ujenzi wa ukuta katika mpaka wa Kenya na Somali utaanza wiki hii.
Kulingana na gazeti la kampuni ya Standard nchini Kenya mji wa Mandera na ule wa Bulahawa hauwezi kutofautishwa kwa kuwa umeshikana.
''Sasa tunataka kujenga ukuta katika eneo la mpakani ili kufunga mpaka kati ya miji hiyo miwili.Hatua hiyo itapunguza watu wanaoingi nchini kenya bila kugunduliwa'',alisema Nkaissery.
Seneta wa mandera Billow Kerro aliunga mkono hatua hiyo lakini akasema kuwa haitaleta suluhu ya kudumu katika eneo hilo.
Amekiri kwamba kuna magaidi wanaotekeleza operesheni zao katika eneo hilo na sio majambazi kama alivyokuwa akisema.
''Tunatumai kwamba ukuta huo utasaidia kudhibiti tatizo hilo '',alisema Kerrow.Amesema kuwa itakuwa vigumu na kugharimu fedha nyingi kuujenga ukuta huo wa kilomita 200 katika mpaka.

No comments: