Sunday, March 22, 2015

ZITTO KABWE AELEZA MIKAKATI KWENYE CHAMA KIPYA. Ajipanga kufyeka msitu!

Aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, ambaye ni mwanachama mpya wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT) (katikati) akzingumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu ajiunge na chama hicho jana. Zitto alisema yupo katika chama kipya amejipanga kufyeka msitu na uwezo huo anao na atatimiza hilo. Aidha zito aliwaambia waandishi hao kuwa hana muda wa kujibizana na watu wanomtupia maneno kwasababu hajalelewa hivyo na siasa za namna hiyo yeye sio zake. Mimi ni mjamaa na husudu sana siasa za Unyerere nimejiunga na chama hichi kutokana na misingi yake kuendana na mambo ninayoyaamini kiuchumi siasa na kiutamaduni. Act kinataka kubadilisha kabisa mwenendo wa siasa za tanzania na watanzania wajiandae kwa hilo.
Zitto Kabwe akisaini kadiyake mpya ya uwanachama wa chama cha ACT jijini Dar es Salaam jana.
Akiwa na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam Dk.Kitila Mkumbo (katikati) mara baada ya kukabidhiwa kadi ya uwanachama.
'Ahsanteni na Kwaherini.'

No comments: