Wednesday, August 26, 2015

Mratibu wa uchaguzi manispaa ya Bukoba amepokea Pingamizi 10 kutoka kata mbalimbali katika ngazi ya udiwani.

PINGAMIZI hizo zimewekwa na wagombea udiwani katika vyama mbalimbali vya siasa, ambapo mratibu huyo wa uchaguzi, Elick Bazombopora, amesema kuwa mgombea wa kata  ya, Kahororo, Chief Abdronicas Kalumuna, amewawekea pingamizi wagombea,  Venant Lugemalila Salapion, wa CCM na Banyenza Saimon, wa  ACT, ambapo hatahivyo, Banyeza amepeleka pingamizi ambalo halikutaja linampinga nani.

Mratibu huyo amesema kuwa katika kata ya miembeni Pingamizi limewekwa na Baganda Gyeshumba Richard, wa CHADEMA akimwekea Richard Gasper, ambapo katika kata Kashai,  mgombea wa CCM Bw Samora Agaptus Lyakurwa, amewekea pingamizi ndugu Kabaju Abdukad, ilhali katika kata Kagondo kuna pingamizi  tano na pigamizi tatu zikiwekwa na Anatory Aman kwa wagombea watatu.

Amesema kuwa amewawekea, Simart Peter Baitan, wa CCM, Joram Ifunya wa CHADEMA, na tatu kwa mgombea wa, ACT ,Benson George Bitegeko, ambapo Joram wa CHADEMA amemwekea Baitan wa CCM, ilhali  Benson George Bitegeko akimwekea Anatory Amani.

Katika barua yake yenye kumbukumbu namba BMC/KT/KAG/A.2/49, amabaye ni msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata Kagondo, amesema kuwa ametengua uteuzi wa, Dr Anatory Amani, kugombea udiwani, kutokana na pingamizi la Bw Benson George Bitegeko wa ACT kuhusu kudanganya eneo alilozaliwa, ambapo katika barua yake Amani alionesha kuzaliwa wilayani Karagwe, ilhali taarifa za mamlaka zinaonesha amezaliwa katika eneo la, Kanoni Rwanda, kwenye wilaya ya Rakai nchini Uganda, hivyo hakutoa taarifa sahihi za kuzaliwa kwake.
Kupitia baraua yenye kumbukumbu KSH/UCH/VEO.1/05, iliyoandikwa na msimamizi kata Kashai, imetengua uteuzi wa ndugu Kabaju Nuruhuda Abdukadir kugombea udiwani kwenye kata hiyo kwasababu ya pingamizi alilowekewwa na mgombea wa CCM ndugu Samora Agapmtus Lyakurwa.

No comments: