Wednesday, October 14, 2015

TAWLA YAENDESHA MIDAHALO YA AMANI, WASHIRIKI WANENA Wasimamizi uchaguzi watende haki.,

Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Sara Kinyaga, akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Baadhi ya washiriki wakimpongeza Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) (kushoto) baada ya kuanzisha mjadala wa amani wakati wa uchaguzi mkuu, wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. 
Ofisa Habari wa Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Goodness Mrema, akielezea muongozo wa mdahalo wa amani kwa wenyeviti, watendaji wa serikali za mita na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani jana, wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya na Mtendaji wa Tarafa ya Chole Wilayani Mkuranga Mkoani Pwani, Asha Risasi, akiwahutubia washiriki wa mdahalo huo.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa makini mdahalo huo.
Baadhi ya washiriki wakimpongeza Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) (kushoto) baada ya kuanzisha mjadala wa amani wakati wa uchaguzi mkuu, wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. 
Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Sara Kinyaga, akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.                                                                   

WASIMAMIZI wa Uchaguzi Mkuu unao tarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu wamehaswa kutenda haki ili kuepusha vurugu ambazo hutokana na haki kutotendeka wakati na baada ya uchaguzi.

Hayo yameelezwa na wakazi wa Kisarawe mkoani Pwani jana wakati wa mdahalo wa amani uliondeshwa na kusimamiwa na Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).
Katika mdahalo huo ambao mada kuu ilikuwa ni umuhimu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

Mada nyingine zilizojadiliwa ni Haki ya mwanamke kushiriki kupiga kura kwnye uchaguzi mkuu, pamoja na elimu ya mpiga kura na Haki za Binadamu.

Akichangi mada wakati wa mdahalo huo ambao ulishirikisha wenyeviti, watendaji wa Serikali za mitaa, Jeshi la Polisi na Watumishi wa halmashauri hiyo, Mwashamba Mrisho,alisema kutokuwepo kwa haki wakati na baada ya uchaguzi ni moja ya vyanzo vya kuvuruga amani.

"Kama haki haitendeki basi ni vigumu sana amani kupatikana, kwa mfano kama watendaji au wasimamizi wa uchaguzi watafanya upendeleo wa kufanya mikutano kwa baadhi ya vyama na kuvinyima haki hiyo kwa baadhi ya vyama kunaweza kubomoa amani iliyopo," alifafanua Mwashamba.

Aidha wananchi hao walibainisha kuwa vyanzo vingine vya vurugu kuwa ni matumizi ya lugha ya matusi pamoja na kutangaza mgombea ambaye hakushinda na kumwacha mgombea aliyeshinda.

Awali akifungua mdahalo huo mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mtendaji wa Tarafa ya Chole, Asha Risasi, alisema kuna umuhimu watendaji wa serikali za mitaa na wananchi kujua majukumu ya Mkuu wa Wilaya kwani wao wako karibu zaidi na wananchi hivyo itasaidia kufanya kazi kwa ushirikiano.

"Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama kwenye Halmashauri ni Mkuu wa Wilaya na yeye ndio mwenye vyombo vya kulinda amani kama Jeshi la Polisi, Takukuru na Magereza, hivyo kuna umuhimu wa wananchi pamoja na watendaji kuelewa hilo ili kurahisisha utendaji wao," alieleza Risasi.

Akitoa nasaha zake kwa washiriki wa mdahalo huo Afisa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo, Constantine Mnemere, alisema kuwa uchaguzi sio vita ni mchakato halali wa kisheria unaolenga kupata viongozi watakao simamia maslahi ya wengi na hakuna sababu ya wananchi kufarakana nakuvuruga amani iliyopo.

Akieleza kwanini wameamua kufanya mdahalo huo kwa watendaji wa serikali za mitaa, watumishi wa Halmashauri na wananchi, Ofisa Habari wa Tawla, Goodness Mrema, alisema kuna kila sababu ya kufanya hivyo katika jamii kwani wananchi wanaingia kwenye uchaguzi wanapaswa kukumbushwa umuhimu wa amani na umuhimu wa kushiriki kupiga kura.

"Tuko atika juhudi za kuimarisha Utawala Bora katika jamii na hii ndio itakuwa chachu ya kuimarisha amani itakayowezesha wananchi kushiriki katika uchaguzi kwa amani na hatimaye kupata viongozi bora," alisema

Aidha Mrema alisema wanafanya midahalo hiyo kwa ngazi ya chini ya uongozi kwakuwa wanaamini kuwa wako karibu zaidi na wananchi na kwakufanya hivyo itasaidia kurahisha kufikisha ujumbe wao.No comments: