Thursday, November 26, 2015

KUBENEA ATEMBELEA MADRASA ILIYOCHOMWA MOTO JANA USIKU, Awashukuru wapiga kura.

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (kulia) akimsikiliza, Diwani wa Manzese ambaye ni Mwalimu na Mmiliki wa Madrasa ya Mus Abu ya Manzese jijini Dar es Salaam leo, baada ya watu wasiofahamika kuchoma moto Madrassa hiyo kwa kunyofoa waya wa dirisha na kupitisha moto kwenye chumba cha kulala wanafunzi. 
Mbunge huyo akiangalia dirisha lililonyofolewa waya na kupitishwa moto ulio teketeza madrasa hiyo.
Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (mwenye miwani) akiwa na baadhi ya viongozi nawafanyabiashara wa soko la Ndizi la Urafiki alipokwenda kuwashukuru kwa kumchagua na kueleza namna atakavyotekeleza ahadi zake.
Akiwahutubia madereva na wafanyakazi wa kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaa leo.

No comments: