Friday, February 5, 2016

BAJETI MANISPAA YA ILALA HADHARANI, Imeongezeka kutoka,Bilioni 30 hadi 55 Bilioni.

Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akizungumza na madiwani wa Manispaa hiyo wakati wa mkutano wa kupanga kamati na mwelekeo wa bajeti ambayo imekuwa juu na kuwaasa madiwani kufanya kazi katika kubuni vyanzo vya mapato.
Baadhi ya madiwani wakifuatilia mkutano huo.
Baraza la Madiwani likiendelea na vikao.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

BAJETI ya Manispaa ya Ilala kwa mwaka wa fedha 2015/2016 ni sh.bilioni 55 kutoka sh.bilioni 30 ya mwaka wa fedha 2014/2016.

Akizungumza katika baraza la madiwani katibu wa baraza hilo na Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi amesema kuwa kutokana na bajeti hiyo kuwa juu madiwani wanatakiwa kufanya kazi katika kubuni vyanzo vya mapato.

Amesema kuwa baraza ndilo linaweza kufanya bajeti hiyo ikatimia katika makusanyo kutokana na vyanzo vya mapato vilivyopo au kuongeza vyanzo vingine.

Mngurumi amesema katika kuanza kufanya kazi kwa baraza la madiwani lazima kamati zipatikane ambapo hilo limefanyika kwa kufanya uchaguzi.

Aidha amesema kuendana na bajeti hizo kamati ziweze kujadili bajeti jinsi ya kuweza kupata bajeti itakayosaidia kuendesha na kutoa huduma kwa wananchi wa manispaa ya Ilala.

Meya wa Manispa kwa ya Ilala, Charles Kuyeko amewataka madiwani kujadili kwa kina bajeti hiyo katika kamati.

01.Mkurgenzi wa Manispaa ya Ilala, Isaya Mngurumi akizungumza na baraza la madiwani juu ya bajeti  kuwa juu madiwani wanatakiwa kufanya kazi katika kubuni vyanzo vya mapato,leo jijini Dar es Salaam.

No comments: