Friday, February 5, 2016

KUTOKA INDIA MCHANA HUU, Tukio la kuvuliwa nguo Mtanzania, Washukiwa zaidi wakamatwa.

Balozi wa Tanzania nchini India John WH Kijazi
Washukiwa zaidi wamekamatwa na maafisa wa polisi nchini India kuhusiana na kisa ambapo mwanafunzi Mtanzania alipigwa na kuvuliwa nguo mjini Bangalore.
Washukiwa wengine wanne wamekamatwa na kufikisha tisa, jumla ya washukiwa wanaozuiliwa na polisi.
Maafisa watatu wa polisi pia wamesimamishwa kazi, wakisubiri kufanyiwa uchunguzi.
Watatu hao wanatuhumiwa kukataa kupokea malalamiko kuhusu kushambuliwa kwa mwanafunzi huyo wa kike wa umri wa miaka 21 pamoja na wenzake wa tatu.
Balozi wa Tanzania nchini India John WH Kijazi anatarajiwa kukutana na waziri wa mambo ya ndani ya jimbo la Karnataka.

No comments: