Thursday, February 4, 2016

LOWASSA AKUTANA NA WAZEE WA CHADEMA, Wateta kwa saa moja! Wazungumzia mikakati mipya.

Aliyekuwa Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, akizungumza na wazee wa Chama hicho Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam leo, walipomtembelea ofisini kwake. Lowassa aliwataka wazee hao kutokata tamaa na kujipanga kimkakati kujiandaa na kuimarisha chama chao pamoja na ukawa kwa ujuml ili kujiandaana uchaguzi ujao wa 2020.
Mmoja wa wazee hao akitoa mawazo yake juu ya namna ya kufanya kabla hawajaingia katika uchaguzi mwingine ili kukabiliana na mbinu za chama ha mapinduzi ili kuwashinda kwenye majimbo mengi zaidi ya sasa.
Mze Enock Ngombale,Ndugu wa Mze Kingunge Ngombale Mwiru ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee wa Chadema jimbo la Ubungo, akiwasilisha mipango na mikakati ya Chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.
LOWASSA ameendelea kuwataka Watanzania kuwa watulivu na kulinda amani ya nchi na kujiepusha na kila jamboambalo wanaona linamwelekeo wa uvunjifu wa amani.

Hayo aliyasema wakati alipokutana na Wazee wa Chama hicho wa jimbo la Ubungo ambao walikwenda kuonananae kwaajili ya kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha Chadema kwaajili ya kujiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020.

Aidha aliwaomba wazee hao kutokata tamaa kwani kuna mambo mengi ya kufanya hadi kufikia malengo waliyojiwekea.

"Hali ya Chama chetu na Ukawa iko vizuri, Uchaguzi Tulishinda sisi tunajuwa, Jumuiya za Kimataifa zinajua na hata CCM wenyewe wanajua kama tulishinda ila ubabe wao na dhulma ndio wamefanya waliyofanya," alisema.

Lowassa alifafanua zaidi kuwa kama chama kinachojiandaa kushika Dola hawakuwa tayari kuingia Ikulu kwa Damu ya Watazania na ndio maana hata vijana walipomtaka atoe kauli ya kuingia barabarani niliwazuia aliwazuia.

Kuhusu sula la mgogoro wa Uchaguzi Zanzibar amewataka CCM kuacha kufanya siasa za Kiimla wasijidanganye kwamba Zanzibar ikichafuka na bara itasalimia.

No comments: