Thursday, February 4, 2016

MAGUFULI ALIPOWAPA DOZI MAJAJI LEO, JIJINI DAR!

Rais Dtk John Pombe Magufuli (kushoto) akisalimiana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman alipo wasili katika viwanja vya Mahakama wakati wa kilele cha Maadhimisho ya 21 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama, Dar es Salaam, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Said Mecky Sadiki .Magufuli alitumia hafla hiyo kueleza shida iliyoko kwenye serikali yake kwa matumizi mabovu ya fedha.

Alitoa mfano wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa NIDA wametumia mabilioni ya Shilingi kwa kwa kutengeneza vitambulisho vya taifa ambavyo viko chini ya kiwango.

Mbali na hilo Magufuli alichukizwa na utendaji wa Polisi na Mahakama kwa kujenga mazingiara ya rushwa kwenye kazi zao na kuhoji, inakuwaje mtu umemkamata na meno ya tembo yako mikononi halafu unasema uchunguzi haujakamilika. 
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) No comments: