Thursday, February 11, 2016

NDONGA ZA RIDHAA NUSU FAINALI YAKAMILIKA LEO, Kesho ni Fainali.

Mabondia wa ngumi za ridhaa Iddi Athumani kutoka Magereza (kushoto) na George Constantine, wakichuana vikali kwenye mashindano ya ngumi za Ubingwa wa Taifa, yanayoendelea kwenye viwanja vya Tanganyika Pakers.
Bondia wa Ngumi za Ridhaa, Said Jabili, kutoka Ngome (kulia), akimtandika konde la kichwa mpinzani wake fadhili Hassan wa JKT, wakati wa mchezo wa nusu fainali ya Ubingwa wa Taifa wa Mchezo huo kwenye michuano inayoendelea viwanja vya Tanganyika Pakers Dar es Salaam jana. Said Jabili alishinda kwa point na kutinga fainali zinazoanza leo. 

No comments: