Thursday, February 11, 2016

OFISI YA MKEMIA MKUU YAPATA VYETI VYA ITHIBATI YA KIMATAIFA.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akiwasili kwenye viwanja vya ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, akiongozana na Balozi wa Japan nchini (kulia) na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Mkemia Mkuu Prof.David  Ngwasaba.
Msimamizi wa Maabara ya Uchunguzi wa Sumu ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Seriali, Domician Mutayoba (kulia), akimuonyesha Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (watatu kushoto) sehemu ya viungo vya binadamu vinavyofanyiwa uchunguzi wa sumu, alipofanya ziara kwenye ofisi hiyo jana. 
Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof.Samwel Manyele (kushoto), akimwonyesha Waziri wa Afya,Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, vyeti vya ithibati vya kimataifa vya vitengo mbalimbali vya Ubora wa uchunguzi wa vinasaba na sampuli mbalimbali. Wengine ni Balozi wa Japan nchini,Masahuru Roshda (kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. David Ngwasaba. 

Gari maalum la wagonjwa wa matukio ya sumu lilikabidhiwa.

No comments: