Wednesday, February 3, 2016

Sheikh Ponda,Amuumbua Sheikh Alhadi, *Asema amemsingizia Sheikh Farid * Hakuna Barua aliyomuandikia.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msimamo wa taasisi hizo juu ya mgogoro wa uchaguzi unaoendelea Zanzibar na kubainisha kuwa hawaungi mkono suala la kurudia uchaguzi. Ponda alikanusha taarifa iliyotolewa na sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam,Alhadi Mussa, kuwa kiongozi wa Uwamsho, Sheikh Farid, anaunga mkono kurejewa kwa uchaguzi wa Zanzibar na kusema amezungumza na Sheikh Farid jana na kukanusha kumuandikia barua Sheikh huyo wa Mkoa.

KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, amemuumbua Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salim, kwa kukanusha taarifa alizozitoa jana kwa waandishi wa habari kuwa Sheikh wa Uwamsho, Sheikh Farid Hadi, ambaye anashikiliwa gerezani Segerea kwa tuhuma za kesi ya ugaidi kuwa ameandika barua kwa sheikh huyo na kumwambia anaunga mkono kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Ponda alisema alikwenda Segerea leo kuzungumza na Sheikh Farid, amekana kuandika barua hiyo na kusema huo ni uzushoi mtupu.

"Leo asubuhi nilikwenda Segerea kabla ya kukutana nanyie hapa, nimezungumza na Sheikh Farid ameshangazwa na taarifa hiyo na kusema kuwa anapokuwa na jambo lolote linalotakiwa kuelezwa kwa jamii anapitia kwa mawakili wake na sio Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam,alisema.

Aidha Sheikh Ponda aliwasiliana na mawakili wa sheikh Farid ambao walimueleza kuwa hawaifahamu barua hiyo anayodai Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam ameandikiwa na Sheikh Farid na kusema hakuna kitu cha namna hiyo.

Akieleza zaidi Ponda alisema ili kutaka kujiridhisha kama kunaukweli wa barua hiyo hakuishia hapo, kwakuwa utaratibu wa kutoa taarifa yoyote ya maandishi gerezani kunahitajika baraka za Mkuu wa gereza, alionana na Mkuu wa gereza la Segerea.

"Mkuu wa gereza hilo alimueleza Ponda kuwa hakuna barua yoyote iliyopitia kwetu hapa na kwamujibu wataratibu zetu hakuna barua inayopasa kutoka hapa gerezani na kwenda uraiani, alisema.

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam jana akizungumza na waandishi wa habari, alidaikuwa kuna barua ameandikiwa na sheikh wa Uwamsho akimtaka kuwaambia Wazanzibari washiriki kwenye uchaguzi na yeye anaunga mkono uchaguzi huo kurudiwa.

Kuhusu uchaguzi wa Zanzibar amesema Jumuiya na Taasisi za kiisilamu haziungi mkono kurejewa kwa uchaguz wa Zanzibar kwani uchaguzi halali ulishafanyika Octoba 25 mwaka janana hakuna sababu yoyote ya kurudiwa kwa uchaguzi.

Aidha alimtaka Rais Magufuli kuepuka lawama zisizo za lazima atekeleze ahadi yake aliyoitoa bungeni ya kushughulikia mgogoro huo wa Zanzibar.

"Kama Zanzibar itachafuka na bara haitasalimika, ni kujidanganya kusema mgogoro wa Zanzibar ni wa Wazanzibari, hivyo basi kunahitajika juhudi za haraka za kutatua mgogoro uliopo badala ya kukimbilia kufanya uchaguzi," alisema.

No comments: