Tuesday, February 2, 2016

WATUMISHI WATAKAO JINUFAISHA WATATUMBULIWA.


NA CATHERIN SUNGURA NZEGA.

SERIKALI haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na kufaidi pesa za walipa kodi hususan wa kipatao cha chini.

Hayo yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo.

Dkt.Kigwangwalla alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini kufanya kazi  za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.

“Serikali haitowavumilia watumishi wazembe, hivyo tutaendelea kuwafungia mageti na kuwashughulikia wale wazembe,tunataka watumishi wa umma wafanye kazi ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi,

mtumishi akizembea tutamtumbua majipu, akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na kumpeleka jela, hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu”

Aidha alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe kazi na kutekeleza ahadi zote za  ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.

“hatutomuonea mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya ya mwaka 2016 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi” alisema.

Hatahivyo aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na hakuna michango yoyote.

“Natoa wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za kuendeshea shule hizo.

Dkt. Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kiini kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.


No comments: