Tuesday, August 9, 2016

KUPATANA DOT COM KUSHIRIKIANA NA TIGO.

Meneja Miradi ya Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Anthony Njau (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa biashara kati ya Tigo na Kupatana.com, Wengine kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao ya Kupatana.com, Philip Ebbersten na Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha.

 Mkurugenzi wa Kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao ya Kupatana.com, Philip Ebbersten  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza ushirikiano wa biashara kati ya Tigo na Kupatana.com,wengine ni Meneja Miradi ya Biashara wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Anthony Njau na mwisho ni Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha 


Meneja mkazi wa Kupatana.com, Makusaro Tesha akifafanua jambo wakati wa mkutano huo mapema leo jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa tigo wakisikiliza kwa makini katika mkutano huo na waandishi wa habari mapema leo katika makao makuu ya Tigo Jijini Dar es salaam,
Kampuni inayoongoza kwa mtindo wa maisha ya kidijitali Tigo Tanzania na kampuni ya Kupatana.com, moja ya kampuni zinazoongoza Tanzania  katika huduma za masoko katika mtandao  zimeingia katika ubia wa kibiashara ambapo kila kampuni  itauza bidhaa na huduma za  kila mmoja katika majukwaa yao ya kidijitali.
Katika hatua za mwanzo za ushirikiano huu, Kampuni ya Tigo Tanzania itachagua maduka matatu ambayo Kupatana.Com itayatumia kuwawezesha wateja wa Tigo kuuza simu zao zilizotumika kwa kupitia jukwaa la Kupatana.com.
Akizungumza wakati wa  kusaini makubaliano baina ya pande hizo mbili jijini Dar es Salaam,  Meneja miradi ya biashara wa Tigo, Anthony Njau alisema, “tukiwa ni kampuni ya mtindo wa maisha ya kidijitali, tumeona kwamba hivi sasa Watanzania wamehamasika mno katika kufanya biashara kupitia njia ya mtandao.”
Njau aliongeza kwamba , “Mtandao na wavuti wa Kupatana.com unatoa jukwaa zuri ambalo linabadilisha  namna ambavyo watu wanaishi kwa kuwezesha kupatikana kwa  huduma na bidhaa katika njia sahihi na rahisi.”
 “Lengo la muda mrefu ni kuwapatia wateja wetu jukwaa  ambalo wanaweza kupakua  vifaa ambavyo vilishatumika ili kuviboresha na kwa upande wa Tigo kuuza  vifaa vipya, kuongeza usambazaji  na kuwa na mafanikio katika  jaribio hili la msingi, Tigo na Kupatana.com zitapanua wigo wa huduma hii na kuhakikisha inapatikana kwa urahisi katika maduka yote 52 ya Tigo  ambayo yamesambaa  kote nchini,” alisema Njau.
 Mkurugenzi wa Kupatana.com, Philip Ebbersten, alisema kwamba kupitia matumizi ya jukwaa hilo, wauzaji (kampuni na watu binafsi) wataweza  kuwafikia maelfu ya  wanunuzi muhimu kila siku bila kujali  maeneo yao ya kijiografia.
Alifafanua kuwa kuorodhesha bidhaa katika jukwaa hilo  ni bure  na kuwashauru wateja umuhimu wa  kufuata kanuni  na miongozo salama kwa bidhaa zote zitakazotangazwa Kupatana.com ili waweze kuzitapa  kwa usalama na uelewa zaidi.

No comments: