Saturday, September 17, 2016

PPF YAWAFUTA MACHOZI WANABUKOBA.

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akikabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, ambayo waliiahidi kwa Msajili wa Hazina kwa ajili ya kuchangia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akizungumza na washiriki wa matembezi ya hisani ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera. Matembezi hayo ya kilomita tano yalifanyika leo viwanja vya Polisi Officers Mess Oysterbay, Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Mfuko huo, kabla ya kuanza kwa matembezi ya hisani ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la ardhi.RAIS Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaji Ali Hassani Mwinyi (katikati) akifanya mazoezi ya viungo kabla ya kuanza matembezi ya kuchangia wahanga wa tetemeko la ardhi lililo tokea mkoani Kagera. Wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, Mbunge wa Muleba Kaskazini, Profesa Anna Tibaijuka na kushotoi ni Waziri wa Mambo ya Njee na Uhusiano wa Kimataifa, Balozi Agustino Mahiga na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Susan Kolimba.
 

No comments: