Wednesday, December 28, 2016

LULU DIVA AFICHUA UKWELI JUU YA KULALA NA BARNABA CLASSIC

Mwanadada ambaye ameingia kwa kasi ya aina yake kwenye game ya Muziku wa Bongo fleva, Lulu Diva, amevunja ukimya na kufunguka kuhusu skendo ya yeye kulala chumba kimoja na msanii Barnaba Classic, walipo kuwa wamekwenda kufanya video nchini Afrika Kusini.
Akifunguka kwa watanzania, Lulu amesema taarifa hizo siyo za kweli na kwamba anamchukulia Barnaba kama kaka yake, hivyo hawezi kumvunjia heshima kwa kuwa na mahusiano naye, wakati akijua kuwa Barnaba anaye mkewake wa ndoa.

“Barnaba na mimi tunaheshimiana sana, tulipokwenda Sauzi hatukufanya chochote, yule ni kaka yangu hata tukiwa chumba kimoja hatuwezi kabisa kufanya chochote, yule ni kaka yangu, kwahiyo taarifa hizo siyo za kweli” Alisema Lulu kwenye FNL.

Kuhusiana na mahusiano yake na mke wa Barnaba amesema wanafahamiana na wanaishi kama marafiki,
“Mimi na mke wake tunafahamiana na ni marafiki wa karibu sana na mambo mengine tunashauriana”.

Amesema kila kitu walicho kifanya kule kilikuwa ni sehemu ya kazi iliyowapeleka kule na si vinginevyo.


No comments: